Featured Articles

Decoration

All Stories

RAY AONESHA JEURI YA FEDHA

NYOTA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ anadaiwa kumpangishia nyumba nzima mpenzi wake ambaye pia anasemekana ni mkewe mtarajiwa, Chuchu Hans, Amani lina picha kamili.
Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa na mkewe mtarajiwa, Chuchu Hans.
Kwa mujibu wa sosi aliye karibu na mastaa hao (jina tunalo), Ray amemwaga shilingi milioni 3,840,000 kwa ajili ya kodi ya nyumba hiyo iliyopo Mwananyamala-Msisiri B jijini Dar es Salaam.
“Wakati wanakwenda kuiona nyumba hiyo kwa mara ya kwanza, ndani ilikuwa imezeeka lakini Ray aliamua kumwaga fedha kwa ajili ya ukarabati na sasa inaonekana ni ya kifahari tena mpya, hata wewe (mwandishi) ukiingia utasema inafaa kukaliwa na staa,” alisema sosi huyo.
Nyumba aliyopangishiwa Chuchu na mumewe mtarajiwa, Ray Kigosi.
MILIONI 1,500,000 UKARABATI PEKEE
Taarifa zaidi zimejianika kwamba, staa huyo alitumia kiasi cha shilingi milioni 1,500,000 kwa ajili ya kufanyia ukarabati nyumba hiyo, kama vile kupaka rangi, kuweka dari mpya, kurekebisha milango sanjari na vitasa, kubandika marumaru na mambo mengine kibao ya kuinakshi, hali iliyowashtua watu wengi.

Nyumba hiyo inadaiwa ina vyumba vitatu vya kulala, sebuleni kubwa, jiko, bafu, choo, stoo na ua mkubwa wa kulaza magari kadhaa (kama anayo).
MASTAA WAMSHANGAA RAY
Wakati staa huyo akidaiwa kuwajibika kwa staili hiyo kwa mpenzi wake huyo, baadhi ya mastaa waliozungumza na gazeti hili walifungukia wakikikejeli kitendo hicho.

Paparazi wa GPL akiongea na hausigeli wa Chuchu.
“Hivi huyu jamaa (Ray) ana akili kweli? Au ndiyo huko kupenda? Anashindwa kuimalizia nyumba yake kule Mbezi (hakusema Mbezi ipi), anabaki kutengeneza nyumba ya watu huku akilipia kodi kubwa,”alisema staa mmoja huku akiomba chondechonde jina lake lisichorwe gazetini.
WAANDISHI MTAANI
Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi wetu walijitosa mtaani kuisaka nyumba hiyo katika maeneo yaliyotajwa ya Msisiri.

CHUCHU HANS NDANI YA BAJAJ
Makadirio ya kiasi cha mita hamsini kufika kwenye nyumba hiyo, Chuchu Hans alitoka na kuingia ndani ya Bajaj yenye rangi nyekundu (namba za usajili hazikupatikana) na kuelekea kusikojulikana.

Mainda.
MAPAPARAZI WAIBAINI NYUMBA
Baada ya Chuchu kuishia, mapaparazi walibaini kuwa nyumba hiyo ndiyo ambayo Ray amejitutumua na kumpangia mrembo huyo.
Nje ya geti jeusi, waandishi walibisha hodi, akatokea msichana aliyejitambulisha ni msaidizi wa kazi za ndani katika nyumba hiyo, yaani ‘hausigeli’.

Paparazi: Tumemkuta Chuchu Hans?
Hausigeli: Hapana. Ametoka sasa hivi.
Paparazi: Amekwenda wapi?
Hausigeli: Mi sijui.

Paparazi: Hakuna mtu mwingine mkubwa mwenye kuweza kuzungumza na sisi chochote?
Hausigeli: Hakuna.
Paparazi: Haya, asante!
Hausigeli: Haya, karibuni.

Johari.
CHUCHU KWENYE SIMU YA MKONONI
Baadaye, Amani lilimpigia simu Chuchu kwa lengo la kutaka kumsikia alichonacho kuhusu nyumba hiyo, lakini simu  hiyo ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

MSIKIE RAY
Kutokana na maadili ya taaluma ya habari, madai hayo ilikuwa lazima pia yamfikie Ray ambaye ndiye anayedaiwa kuonesha jeuri ya fedha.
Paparazi: Mambo Ray?
Ray: Poa, mzima?

Paparazi: Mi mzima tu.
Paparazi: Ee bwana, hapa ni Global Publishers, kuna ishu nataka kujua. Tumepokea habari kwamba umempangia nyumba Chuchu pale maeneo ya Mwananyamala Msisiri. Labda tuanzie hapo, ni kweli madai hayo?
 Ray: No comment (akakata simu).

Nyumbani kwa Chuchu.
JOHARI AZIDI KUKONDA
Vuguvugu la Ray na Chuchu kuwa wapenzi, kumesababisha kuharibu mfumo wa maisha ya watu waliodaiwa tangu zamani kwamba ni wapenzi wake, Blandina Chagula ‘Johari’ na Ruth Suka ‘Mainda’.
Kuzidi kupungua uzito kwa Johari kunatajwa kuwa chanzo ni Ray kummwaga yeye na kuhamishia kambi kwa mwanadada huyo. Amewahi kuulizwa kuhusu hilo lakini amekuwa mgumu wa kusema ukweli licha ya kwamba za chini ya kapeti kwa mastaa zinakiri hilo.

Kwa upande wake, Mainda alipoulizwa na Amani kuhusu anavyojisikia Ray kuwa na Chuchu alifunguka yote (yaliandikwa kwenye Gazeti la Risasi Mchanganyiko). Lakini mwisho wa maneno yake yote ni kumwachia Mungu na kwamba, ameshaamua kuishi kivyake akimwona ‘zilipendwa’ huyo kama alimpotezea muda.
11:05 PM - By Unknown 0

POZI LA MASOGANGE NA MWANAUME UTATA TU

PICHA mpya ya ‘video queen’ matata Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’ na mwanaume mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja, imezua utata kutokana na ukaribu wao.
Agnes Jerald ‘Masogange’ katika pozi na mwanaume ambaye hakujulikana jina lake.
Picha hiyo ilitupiwa katika mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki iliyopita huku ikisindikizwa na maneno kuwa wawili hao ni wapendanao hali iliyosababisha wadau wengi kupongeza kuwa ni kapo nzuri.
“Mh! Kapo nzuri jamani, atulie sasa hapa Masogange,” mmoja wa wachangiaji alipongeza. Alipotafutwa Masogange kwa njia ya simu, hakupokea! Jitihada zinaendelea kuondoa utata huo.
11:01 PM - By Unknown 0

LINAH: WANAUME WAFUPI SIYO ‘UGONJWA’ WANGU

Esterlina Sanga ‘Linah’.
Na  Mayasa Mariwata
MWANADADA mwenye sauti tamu kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Esterlina Sanga ‘Linah’ amesema katika maisha yake kamwe hafikirii kuja kuolewa na mwanaume mfupi kwani siyo sampuli yake.

Akipiga stori na paparazi wetu juzikati, Linah alisema atakuwa si mkweli akitamka ana mwanaume mfupi kwani hata jamii itamcheka kwa kuwa hata Amini Mwinyimkuu aliyewahi kuwa mpenzi wake ni mfupi.
“Nisiongee uongo kusema eti sipendi kutoka kimapenzi na mwanaume mfupi wakati nilishawahi kufanya hivyo na siwezi kujiapiza katika hilo, ila kwenye swala la ndoa lazima nizingatie kigezo changu  muhimu cha kuolewa na mwanaume mrefu,” alisema Linah.
10:57 PM - By Unknown 0

SHILOLE: BABY MADAHA HAJIELEWI

STAA wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amemfungukia msanii mwenzake, Baby Joseph Madaha kwamba  hajielewi.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Shilole ametoa kauli hiyo siku chache baada ya kuchanwa gazetini na Baby Madaha kwa kuambiwa kuwa yeye ni mcheza vigodoro.
Baby Joseph Madaha.
“Sitaki kabisa kumsikia huyo Baby Madaha, hanisaidii chochote kile katika maisha na kazi zangu pia sioni sababu ya kupigizana naye kelele, mtu mwenyewe hajielewi,” alisema Shilole.
10:54 PM - By Unknown 0

MASKINI JACK... HALI MBAYA....NI BAADA YA KUKWAA GONJWA LA AJABU MAHABUSU

MODO mwenyemvuto Bongo Jacqueline Patrick ‘Jack’, ambaye yuko mahabusu ya Gereza la Qincheng nchini China kwa madai ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini humo, anazidi kuteseka, safari hii akidaiwa kukabiliwa na tatizo kubwa la kiafya.
Jacqueline Patrick ‘Jack’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jack anasumbuliwa na ugonjwa wa kukosa hamu ya kula, hali iliyomfanya apoteze uzito wa kilo kumi huku akikabiliwa na tatizo lingine la kupungua kwa kasi ya mapigo ya moyo.
KAMA HALI ITAENDELEA
Chanzo kimesema kuwa endapo hali ya kuzorota kwa afya hiyo kutaendelea, Jack anaweza kujikuta katika tatizo kubwa zaidi ambalo linaweza kusumbua kwenye mwenendo mzima wa kesi yake.

“Kusema kweli kuhusu maisha ya mahabusu si mabaya sana kwake, hateswi kwa kupigwa wala hanyimwi chakula, ila hana uhuru binafsi, ni kama amefichwa, naamini matatizo hayo ya kiafya yanatokana na uzito wa kesi yake,” kilisema chanzo hicho.
MLOLONGO WA MAMBO
Habari zaidi zinadai kwamba kesi ya msingi ya staa huyo kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya itaanza kusikilizwa rasmi Septemba, mwaka huu baada ya mwanasheria wake kukamilisha taratibu zote.
“Ile kesi yake sasa ni Septemba mwaka huu. Si unajua hajawahi kupandishwa kizimbani kuulizwa kama ni kweli alikamatwa na unga au la!” kilisema chanzo hicho.

Jack Patrick akiwa amefunikwa uso baada ya kukutwa na pipi za heroin tumboni nchini China.
WAKILI WAKE ANATOKA HONG KONG
Taarifa zaidi zinasema kuwa wakili wa mrembo huyo anatoka jijini Hong Kong nchini humo ambako ndiko kwenye wanasheria wazuri kwa kiwango cha kesi yake ya unga.

KUMWONA NI KWA AHADI
Ikazidi kudaiwa kwamba kuna Mtanzania mmoja tu ambaye amekuwa na fursa ya kumuona modo huyo na kabla ya kwenda lazima aombe na kupewa ‘apointimenti’ maalum.

WALIOMTUMA WAMPIGA CHENGA, WALA ‘BATA’
Tofauti na kwa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye naye aliwahi kupata msala mkubwa kama huo nchini Afrika Kusini, Julai, mwaka jana ambapo ‘mabosi’ wake walikuwa mstari wa mbele kumhangaikia, Jack anasota mwenyewe.

Habari zinasema kuwa hakuna cheni yoyote kutoka kwa watu ambao wanatafsiriwa kuwa ni waliomtuma kwani wanaosumbuka ni watu wake wa karibu, wakiwemo ndugu zake.
Juzi, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na mtu wa karibu sana na mtuhumiwa huyo ambapo alikiri Jack kuwa na hali ngumu katika kesi yake hiyo huku akisema kwamba watu wanaodaiwa ndiyo mabosi wake wanakula ‘bata’ tu jijini Dar es Salaam.
“Unajua tatizo la biashara ya unga ni hapo tu! Wewe unayebeba ukinaswa ni juu yako, waliokutuma wao wanachofanya ni kuthibitisha tu kuwa ni kweli umekamatwa maana wapo wanaodaiwa wamekamatwa kumbe si kweli, wanaingia mitini na mzigo,” alisema mtu huyo.  
SABABU ZA MOYO KUSHINDWA KUSUKUMA DAMU
Juzi, gazeti hili lilimtafuta daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo) na kumuuliza tatizo la moyo kushindwa kusukuma damu ambapo alisema:

“Moyo kushindwa kusukuma damu kwa mwendo wa kawaida husababishwa na shinikizo la damu lisilodhibitiwa, mgonjwa kushindwa kudumisha udhibiti wa maji mwilini, chakula au dawa.
“Sababu nyingine ni upungufu wa damu na utoaji wa kiwango cha juu cha homoni za koromeo ambazo zinaleta maumivu ya ziada kwenye misuli ya moyo, utumiaji mwingi wa vimiminika au ulaji wa chumvi uliopitiliza na utumiaji wa dawa ambazo husababisha uwekaji wa maji mwilini kama vile Hiazolidinedione.”
KUHUSU KUKOSA HAMU YA KULA
Kwa mujibu wa daktari huyo, tatizo hilo humkumba mtu anapokuwa katika msongo mkubwa wa mawazo kutokana na jambo zito linalomkabili, ambalo halina mlango wa kutokea.

TUKUMBUKE
Mrembo huyo alikamatwa Desemba 19, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Macau, China akitokea Bangkok, Thailand akiwa na kete 57 (kilo 1.1) za heroin tumboni zikiwa na thamani ya jumla ya zaidi ya shilingi milioni 300.

Awali ilidaiwa kuwa kesi yake ingeanza kusikilizwa mwaka 2016 baada ya yeye kujifunza Kireno (lugha inayotumika Macau) kwa miaka miwili.
2:51 PM - By Unknown 0

LULU MICHAEL ANASWA AKIPIGWA MABUSU NA KUSHIKWASHIKWA KIMAHABA NA MWANAUME USIKU WA MANANE



 
Star aliyejaaliwa kipaji cha kuigiza  almaarufu  kwa  jina  la  Elizabeth Michael  "Lulu  Michael " amenaswa akipigwa mate  na kushikwa kimahaba  usiku  wa  manane ndani  ya  vichochoro  vya  jiji  la  Dar  na jamaa ambaye hakujulikana jina lake mara moja. 

Hivi karibuni ilidaiwa kuwa Lulu alipata mchumba ambaye siye huyo anayeonekana pichani hapo juu,  kwa hiyo uchumba wake unaweza kuwa hatarini kwani kwa mapozi aliyoweka na jamaa   huyo inaonekana ni watu waliozoeana  KIMWILI.
2:25 AM - By Unknown 0

WEMA AMHARIBIA PASTOR MYAMBA


Wema Sepetu.
STAA wa filamu mwenye jina kubwa nchini, Wema Sepetu hivi karibuni alimuharibia siku Emanuel Myamba maarufu kama Pastor Muyamba, kwa kushindwa kufika kwenye hafla iliyokuwa imeandaliwa na chuo chake cha sanaa ‘TFTC’ akiwa kama mgeni rasmi.
Mtoa habari wetu ndani ya taasisi hiyo aliliambia gazeti hili kuwa, Wema aliombwa na kukubali kuhudhuria shughuli hiyo, lakini alipopigiwa simu dakika za mwisho aliwaambia kwamba atashindwa kufika kwa kuwa amefiwa na shangazi yake udhuru ambao baadaye ulibainika kuwa haukuwa wa kweli.

Alisema kutokana na kutofika kwa staa huyo, ambaye hata hivyo mwaliko wake ulitokana na shinikizo la wanafunzi wa chuo hicho, walilazimika kuwaomba radhi wageni wengine, wakiwemo waandishi wa habari.
Emanuel Myamba 'Pastor Muyamba'.
Mmoja wa watu wa karibu na Wema aliliambia gazeti hili kuwa muigizaji huyo hajawahi kupatwa na msiba siku za hivi karibuni, kwani mara zote amekuwa akiwaeleza kila linapotokea jambo zito kama hilo.
Mtu huyo alisema katika ratiba ya siku hiyo, walikuwa waende kwenye tukio moja la starehe na halikuwa limebadilika.
juzi alipoulizwa Pastor Myamba alikiri Wema kutofika kwenye hafla hiyo kitendo alichosema kimemsikitisha kwani walitoa mwaliko kwake kutokana na heshima aliyonayo.
“Nimemshangaa sana, lakini mbona mwenzake Jokate alikuja, ni kwa sababu anajitambua na ni professional,” aliema Myamba.
2:22 AM - By Unknown 0

LINNAH AFUNGUKA MAZITO,,, ADAI ALISHAWAHI KUDUU NA MZUKULE

Chanzo cha habari hii kilipata nafasi ya kuongea na msanii Linah sanga na haya ndiyo mambo matano yanayomuumiza hadi leo...

1. “nilivyosikia boyfrend wangu amenidanganya nilijisikia vibaya, unajua ni mtu ambaye sikutegemea kabisa. Tupo pamoja miaka yote na yupo so sweet kwangu lakini sikutegemea jinsi nilivyosikia eti ana-cheat baada ya mambo yote tuliyopitia,kwakweli zile taarifa zilinifanya niwe down sana”

2. “Nilivyokua form four majibu yalivyotoka , unajua mimi nilikua na plan za kusoma na kufika mbali.Sometime nakumbuka matokeo yalinifanya nisiwe na raha kabisa na kuna wakati mambo ya muziki yakienda vibaya najuta sana nakumbuka zile siku” 
3. “Hadi sasa nafanya kazi ya muziki but i’m not happy kwasababu najua nawaudhi wazazi wangu. wazazi wangu wanatamani siku moja nirudi kundini (kanisani) lakini sasa mimi nafanya muziki in a good way na bado naendelea kua binti mzuri kwa wazazi wangu” 
4. “Niliwahi kum-date mtu ambaye hakuwa sawasawa kama binadamu wa kawaida. yule kaka alikua na miaka 24 na mimi nina miaka 15 kwa wakati ule na historia yake huko nyuma alipitia mambo ya kishirikina akawa kama msukule. kipindi kile kilikua kigumu sana kwangu” 5 . “Niliwahi kuumwa sana na kukaribia kua chizi kutokana na mahusiano . sehemu pekee niliyoponea ilikua ni kanisani kwa maombi ya muda mrefu sana.siwezi kusahau kipindi kile na hadi leo namshukuru mungu kwa kupona.”


5 . “Niliwahi kuumwa sana na kukaribia kua chizi kutokana na mahusiano . sehemu pekee niliyoponea ilikua ni kanisani kwa maombi ya muda mrefu sana.siwezi kusahau kipindi kile na hadi leo namshukuru mungu kwa kupona.”
2:28 AM - By Unknown 0

DAVIDO AWABEEP WATU ATUPIA PICHA INSTAGRAM AKIMKISS DEMU NA KUIDELETE MUDA HUO HUO

Davido himself shared the photo on his instagram page but deleted it almost immediately. Anyone know who the girl is?
12:34 AM - By Unknown 0

SUPERSTAR WA KIKE WA HOLLYWOOD AVAA NGUO YA AIBU WAKATI WA KUSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA

She claimed to feel like a 'princess' as she celebrated her 33rd birthday at the weekend.
However, reality star cum Hollywood actress, Paris Hilton shouldn't accept a Royal invitation anytime soon.
The blonde socialite opted for a very revealing outfit for her birthday bash as she walked the red carpet.
We really hope someone bought miss Hilton some new underwear as a gift because the poor lass seems to be in dire need of some new pants after going commando on Sunday night.
Paris narrowly avoided a major wardrobe malfunction of epic proportions as she posed for photos at Greystone Manor.
She struggled to keep her flowing pink dress in place and just about managed to keep herself covered up.
But it was obvious that the Hilton hotels heiress had forgotten to wear her underwear as she flashed just a little more flesh than she (probably) bargained for.
Earlier in the evening Paris tweeted: "Love my beautiful #Birthday dress! Thank you alonlivne! I feel like a princess!!"
Hmmm, we wonder if she feels the same way after seeing these photos?
12:14 PM - By Unknown 0

KABAMBE

© 2014 SWAGGA ZA BONGO. Distributed By MyBloggerThemes | Design By Bloggertheme9
Powered By Blogger.
back to top