NILIMFUMA MKE WANGU AKINYATIA KUINGIA KWENYE CHUMBA CHA MDOGO WANGU WA KIUME AKIWA NUSU UCHI.

1:52 PM - By Unknown 0


 
 
Kumbe ilikuwa ni tabia yake kwenda kwa mdogo wangu huyo wa kiume ambaye ni mtoto wa shangazi yangu, na kula uroda wakati mimi sipo, nilipata tetesi hizo kutoka kwa housegirl wetu lakini sikuweza kuamini. siku hiyo nilirudi kimya kimya na kujifungia chumba kimoja ambacho kilikuwa hakitumiki, na wote hawakujua kama nilikuwa nipo.


Mara ilipofika ,majira ya saa nne hivi usiku, nilimuona mke wangu ananyata huku akiwa amevaa nguo za ajabu sana, alipita chumba cha house girl na kisha kuzama kwenye chumba cha ndugu yangu huyo wa kiume. nilitoa simu yangu niliyokuwa nayo na kumpiga picha kwa ushahidi zaidi, alipoingia tu na mimi nikaingia alishindwa kuamini na gafla alianza kuomba msamaha, nilimuuliza mke wangu kwani umefanya nini alishindwa kunijibu huku akiendelea kulia na kuomba msamha, nilitoka na kwenda chumbani kwangu kulala, yule mdogo wangu wa kiume alifungasha usiku ule ule na kuondoka na mke wangu hakuweza kulala, iliniuma sana sikuweza kuamini kwani nilimuamini sana mke wangu.

Kesho yake sikuweza kuvumilia nilichukua uamuzi wa kumrudisha kwao , kwani ningeweza kumfanya kitu kibaya sana kama ningeendelea kumuona.

Tags: ,
About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Follow me @Bloggertheme9
View all posts by admin →

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

0 comments:

KABAMBE

© 2014 SWAGGA ZA BONGO. Distributed By MyBloggerThemes | Design By Bloggertheme9
Powered By Blogger.
back to top