KAJALA ALEWA TILALILA NA KUGEUKA KITUKO

3:49 AM - By Unknown 0

STAA wa sinema za nyumbani (Swahili Hood), Kajala Masanja amegeuka kituko nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu, Kijitonyama, Dar baada ya kulewa tilalila na kuwaacha midomo wazi wasanii wenzake.
Kajala Masanja.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Kajala alifanya madudu hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akirekodi filamu yake inayokwenda kwa jina la Laana ambapo waigizaji wenzake walikuwa nje wakisubiri atoke aanze ‘kushuti’ kumbe alikuwa kaegemea mlango huku akiangua kicheko bila kujua afanye nini.
Ilisemekana kuwa baada ya maji kuzidi unga, mwongozaji wa filamu hiyo, Leah Ndemesamkye ‘Lamata” ilibidi ashikwe na kigugumizi baada ya kuona mauzauza hayo ya Kajala na kumuuliza ni kitu gani ambacho kimempata kwani kila anachoongea naye, yeye anaishia kucheka mfululizo.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lilimvutia waya Kajala ili kudhibitisha madai hayo ambapo Kajala alikiri kulewa kidogo na kumtupia mpira rafiki yake kipenzi Wema kuwa ndiye aliyemnywesha.
Alisema: “Unajua nini, siku hiyo tulilala kwa Wema, ndiye aliyeninywesha pombe lakini mbona kazi iliendelea kama kawaida jamani?”

Tags: ,
About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Follow me @Bloggertheme9
View all posts by admin →

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

0 comments:

KABAMBE

© 2014 SWAGGA ZA BONGO. Distributed By MyBloggerThemes | Design By Bloggertheme9
Powered By Blogger.
back to top