STAA wa sinema za Kibongo, Flora Mvungi amesema maisha ya kuoana staa kwa staa yanadumisha uaminifu na ndiyo maana anajisikia furaha kuolewa na Hamis Baba ‘H-Baba’, staa wa Bongo Fleva.
H-Baba na mkewe Flora Mvungi wakilishana keki wakati wa bethidei ya H-Baba hivi karibuni.
Akipiga stori na Stori 3, Flora alisema maisha anayoishi yeye ni tofauti sana na maisha wanayoishi wanandoa wengine, ni matamu kwa kuwa hakuna ugumu wa kumuelewa mwezi wako katika majukumu yake ya kikazi hata kama itamlazimu kukaa kambini.“Ujue wasanii wenzangu hawajagundua tu hicho kitu, ni raha sana mkioana wote mnafanya sanaa iwe muziki au filamu, hata kama mmoja shughuli zimembana ikamlazimu kulala nje na nyumbani ni rahisi mwenzako kukuelewa,” alisema Flora.
About the Author

0 comments: